Kituo cha AzamTV kupitia AzamTV NEWS kimefanya mahojiano na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai kutaka kujua kuhusu kujiuzulu kwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu.
Mtangazaji Charles Hillary akimuhoji Spika alisema hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita kwa Mbunge kujiuzulu kwa hiari yake, Spika Ndugai alijibu>>> “Sijapokea barua yoyote ile yenye kuzungumzia habari za kujiuzulu”
Mtangazaji huyo alipouliza, nini kitachofata baadae kwa Mbunge huyu… Spika alijibu >>> “inakua vigumu kuongelea swala hili kwa sababu hajaniandikia kujiuzulu, bado sijapata barua yake kwahiyo kwenye madaftari yangu namuhesabu bado ni Mbunge kamili mwenye haki zake zote“
“Labda nimshauri tu kwamba kwa wazo hili ambalo na mimi nimelisikia kwenye vyombo vya habari, basi afanye hima aniletee waraka wake huo uwe ni wa kwake kweli ili niweze kufanyia kazi lakini pili amuandikie barua Katibu mkuu wa CCM kumfahamisha hili la kuachia Ubunge na hizo nafasi nyingine ndani ya chama”
SWALI: Iwapo barua itakufikia kesho mapema asubuhi nini utakachofanya?
JIBU: “Nisingependa sana kusemea jambo ambalo sijalipata lakini utaratibu ni kwamba aniletee hiyo barua, ilikua ni vyema kama angeniletea kwanza kabla ya kufanya alichokifanya lakini sio nia yangu kumlaumu“
“Akishaniletea na nikathibitisha kweli kwamba ni ya kwake na yeye akanithibitishia basi hapo ndio nitakaa na timu yangu na Wataalamu wangu kuweza kuona hatua zinazofata”
SWALI: Kawaida Mbunge akijiuzulu Ubunge inamaanisha Ubunge ameupoteza, kitakachofata kwenye jimbo lake ni uchaguzi, yeye Nyalandu ataruhusiwa kugombea katika chama ambacho atakwenda??
JIBU LA NDUGAI: “Katika demokrasia ya kawaida mi naamini anaruhusiwa mradi atekeleze zile sifa ndani ya katiba ambazo zinamruhusu kugombea na sifa moja wapo lazima awe na chama cha siasa”
ULIPITWA NA KAULI YA LAZARO NYALANDU KUJIUZULU? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA MWENYEWE
VIDEO: Mama alieangua kilio mbele ya Rais Magufuli Mwanza, bonyeza play hapa chini kuona maagizo ya Rais Magufuli