Kevin De Bruyne anaweza kurejea baada ya kuchaguliwa katika kikosi cha Manchester City kwa ajili ya Kombe la Dunia la Vilabu mwezi huu nchini Saudi Arabia.
FIFA Jumatano ilitoa vikosi rasmi vya wachezaji 23 kwa ajili ya michuano hiyo itakayoanza Desemba 12, na uwepo wa jina la De Bruyne ulidhihirika.
Mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 32 hajashiriki katika kikosi cha mabingwa hao wa Uingereza na Ulaya tangu afanyiwe upasuaji wa nyama ya paja mwezi Agosti. Hivi karibuni alisema ahueni yake inaendelea vizuri lakini hatarajii kurejea uwanjani hadi mwakani
Ikiwa De Bruyne atakuwa fiti vya kutosha kushiriki Jeddah bado haijajulikana, ingawa inaweza kuwa fursa kwake kurejea kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza kwenye kambi ya hali ya hewa ya joto.
City, ambayo inawakilisha Ulaya kama mshindi wa Ligi ya Mabingwa, haitaingia katika Kombe la Dunia la Klabu hadi hatua ya nusu fainali. Timu hiyo imepangwa kucheza Desemba 19 dhidi ya mshindi wa mechi kati ya Club Leon ya Mexico na Urawa Reds ya Japan.
Fainali ni Desemba 22.