Roberto de Zerbi huenda akaondoka Brighton msimu huu wa joto lakini anadai kuwa bado hajapanga chochote.
Kocha huyo wa zamani wa Shakhtar Donetsk aliiongoza klabu hiyo hadi nafasi ya sita msimu uliopita na kuisaidia kutua soka la Ulaya kwa mara ya kwanza.
Lakini amechagua kusonga mbele kwa changamoto mpya na gazeti la Bild linaripoti kwamba yeye ndiye chaguo la kwanza kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel huko Bayern Munich.
“Hakuna klabu yoyote — hakuna aliyetoa [chochote]. Kwa sasa, hakuna,” De Zerbi alisema.
“Natumai kufanya kazi katika Ligi ya Premia tena. Sijui wapi au lini. Lakini ilikuwa heshima kufanya kazi katika Ligi Kuu.”