Pamoja na kuwa Liverpool waliruhusu kufungwa goli kipindi cha kwanza dakika ya 25 na Luis Suarez katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya UEFA Champions League dhidi ya FC Barcelona, Liverpool walionesha uhai mkubwa kiasi cha kuielemea Barcelona ambayo ilikuwa nyumbani.
FC Barcelona walionekana kuzidiwa zaidi na Liverpool katika eneo la kiungo lakini baadae Lionel Messi aliamua matokeo ya mchezo huo kwa kubadilisha hali ya hewa ghafla baada ya kufunga magoli mawili ya ushindi dakika ya 74 na 81 na kuufanya mchezo huo uliyochezwa May 1 2019 kumalizika kwa Barcelona kupata ushindi.
Matokeo hayo sasa yataifanya FC Barcelona isafiri hadi Anfield kutafuta sare, ushindi au kufungwa kwa chini ya magoli matatu ili waingie fainali, Lionel Messi ameendelea kuwa na kumbukumbu nzuri na siku ya May Mosi baada ya kufanikiwa kusherehekea kipekee siku hiyo, Lionel Messi mara ya kwanza kuifungia Barcelona goli lake la kwanza ilikuwa May 1 2005 lakini leo amefunga goli lake la 600 akiichezea Barcelona katika siku kama hiyo, hivyo unaweza kusema Messi ana historia na siku hiyo.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania