Baraza la Katiba la Chad limemtangaza rais wa mpito Mahamat Idriss Deby Itno kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Mei 6 kwa asilimia 61 ya kura.
Siku ya Alhamisi, baraza hilo lilikataa rufaa zilizowasilishwa na upinzani, ambao ulidaiwa kuwa mshindi halali wa uchaguzi huo, kwa sababu ya wizi wa kura.
Mgombea mkuu wa upinzani Succes Masra, aliyeibuka wa pili kwa 18.5% ya kura, alikuwa amepinga ushindi wa Deby baada ya bodi ya uchaguzi kutangaza matokeo Mei 10.
Chad imekuwa nchi ya kwanza kati ya nchi zilizokumbwa na mapinduzi katika Afrika Magharibi na Kati kurejesha sheria ya kikatiba kupitia sanduku la kura.