Mkurugenzi mtendaji wa REPOA ,Dr.Donald Mmari leo ametia saini Mkataba wa ushirikiano na Ubalozi wa Denmark.
Mkataba huu umesainiwa na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mette Norgaard, ambapo serikali ya denmark itaipatia Billion 1 taasisi ya Repoa.
Mbali na hilo Dr.mmari amesema aina za utafiti zitajikita kuangalia namna ya kuongeza uzalishajj wa bidhaa ambazo zimekuwa zikiagizwa kutoka nje ya nchi, hili litasaidia kuwa tayari na majanga yote yatakayotokea.
Kwa upande wake balozi wa Denmark nchini TZ Mette Norgaard alisema kama ilivyo kwa nchi nyingine Serikali na watunga sera watanzania wanahitaj kupata aina za tafiti zilizo bora na zilizochambuliwa kwa kina ili kusaidia kwenye uaandaaji wa mipango,kuendeleza sera za uchumi na ufwatiliaji wake.
Alisema kutokana na uhalisia huo serikali yake imeona ni vyema kuwekeza katika eneo hilo kwenye taasisi ya Repoa.