Nchi ya Denmark imesitisha utoaji wa Chanjo ya Oxford-AstraZeneca kwa muda wa wiki mbili ili kuchunguza ripoti za baadhi ya wagonjwa kupata tatizo la damu kuganda siku chache baada ya kupatiwa chanjo hiyo..
Waziri wa Afya nchini humo amesema wamechukua hatua hiyo ikiwa sehemu ya tahadhari ili kuchunguza endapo kuna madhara zaidi yaliyojitokeza tofauti na la damu kuganda.
Mamlaka ya Afya ya Denmark imesema uamuzi wa kusimamisha chanjo umekuja baada ya mwanamke wa miaka 60 nchini humo kupewa dozi ya AstraZeneca na kupoteza maisha.