Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema wamemkamata Dereva wa Lori Joseph Zacharia ambae anadaiwa kusababisha ajali iliyoua Watu sita na kujeruhi wengine 12 ikihusisha Lori na Coaster.
Muroto amesema Dereva wa Lori alikuwa analikwepa shimo na akaparamia Coaster ambayo ilikua kwenye eneo lake na kufumua paa ya juu kisha ajali ikatokea, baida ya ajali Dereva huyo alitoroka lakini wamemkamata.
“Sielewei nini kilitokea nilikuwa kwenye Coaster usingizi ulinipitia, kushtuka naona Watu wamemwagwa nikasikia wasaidie hao wengine wazima” -Frank Lyimo, Majeruhi