Halima Sheikh Mbwana dereva aliyepata ajali Wilayani Tunduru na kukatika mkono akiendesha Basi ya Super Feo amefanya mahojiano maalum na Ayo TV akiwa hospitalini St.Benedict Mkoani Mtwara alipolazwa.
Pamoja na kwamba amekatika mkono, Halima amekiri kwamba atarudi kazini “Nikipona nitarudi hata kama kuwa Kondakta au Wakala ila nitarudi kufanya ile kazi naipenda sana”
“Nilipigania gari lisilale Barabarani kwasababu nilijua majeraha na vifo vitakuwa vingi mpaka nilisimamia usukani gari ikaenda kulala mlalo baridi kwenye majani, wakati nahangaika kurudisha usukani mkono ulichomoka ukakatwa na kioo cha dirisha la mlangoni, umekatwa kwenye vidole mpaka juu ya kifundo cha kikunjio ndio ambako nilisagika”-
“Nikazima gari kwa mkono wa kushoto nikaweka stop engine ili kukata umeme lisilipuke, Nawashukuru Watanzania, Mama Samia ujumbe wake nimeupata amenipa moyo kwamba hatutakiwi kukata tamaa, namshukuru Waziri Gwajima amenionesha ushirikiano, pia naushukuru uongozi wa Yanga wamenionesha ushirikiano Shabiki yao, Manara nimepata ujumbe wake”
Unaweza kumpa support Halima kupitia namba 0717770389 (Esther Kambona) au
0626452699 (Saadia Mbwana).