Dereva wa Treni iliyobeba watu 160 Nchini Japan anakabiliwa na adhabu baada ya kuachia nafasi yake kwa dakika kadhaa ili kwenda kujisaidia.
Dereva huyo wa miaka 36 aliumwa tumbo na alihitaji kwenda maliwatoni haraka hivyo alimuita kondakta asiye na leseni ya udereva na kumuachia treni kwa dakika tatu. Wote wawili wanakabiliwa na adhabu.
Reli za Japan zinasimamiwa kwa viwango vya juu vya usalama na mara ya mwisho ajali kubwa kutokea ilikuwa mwaka 2005 ambapo watu 107 walifariki dunia.