Polisi Mkoa wa Arusha limewakamata watatu ambapo wawili wakiwa dereva na ofisa uhamasishaji wote wa CHADEMA wanaotuhumiwa kuhusika na tukio la kuchoma moto Ofisi za CHADEMA Arusha Agosti 14, 2020.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Salum Hamduni, ambapo amesema kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea, uchunguzi wa kina ulifanyika kuwabaini na kuwakatama watu wote waliohusika katika tukio hilo ambapo Agosti 19 alikamatwa mlinzi wa Ofisi hiyo aitwaye Deogratius Malya.
Mbali na huyo Jeshi hilo pia limemkamata Leonard Cathbert Ntukula, ambaye ni Dereva wa CHADEMA na Mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam, pamoja na Prosper Masatu Makonya, ambaye ni Afisa mhamasishaji wa CHADEMA Makao Makuu na Mkazi wa Makongo Jijini Dar es Salaam, ambao wote hao walikamatwa kati ya Agosti 28 na 29 mwaka huu.
MAJAMBAZI 7 WATEKA GARI LENYE ABRIA 11 ”WAMEPORA MILION MOJA NA SIMU NANE”