Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2023 yamebebwa na kauli mbiu isemayo “Jamii iongeze kutokomeza UKIMWI” ambapi kilele cha maadhimisho ya UKIMWI Duniani kwa mwaka huu kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro.
Katika mkoa huo umevuka malengo ya tisini na tano tatu (95, 95, 95) hadi kufikia mwezi Septemba 2023 Mkoa umevuka malengo katika mapambano dhidi ya maambukizi ya UKIMWI kwani Tisini na tano ya kwanza (wananchi wanaotambua hali zao za maambukizi ya VVU baada ya kupimwa ni asilimia 98.8%), Tisini na tano ya pili: (wanaotumia dawa kati ya watu waliogundulika kuwa na VVU ni asilimia 95%) na Tisini na tano ya tatu (inaonyesha kuwa kati ya watu wanaoishi na VVU ambao wanatumia dawa za ARV wamefubaza VVU ni asilimia 95.8%).
Jitihada zilizotumika katika kupunguza maambukizi mapya ya ugonjwa huo ni pamoja na kutoa ushauri nasaha na upimaji wa hiari, matunzo na matibabu kwa watu wanaoishi na VVU (WAVIU).
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na ujumbe wa mwaka huu unasema Wekeza kuzuia ukatili wa Kijinsia.
UKIMWI uligundulika Wilayani Kilosa mwaka 1998 ikiwa ni miaka 35 iliyopita tangu mgonjwa wa kwanza kupatikana Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.
Hadi sasa jumla ya watu 71,979 wanaishi na VVU Mkoani Morogoro.