Kutokea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo March 8, 2018 imeelezwa kuwa afya ya Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva sio nzuri na amelazwa kitengo cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tangu jana.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Aveva, Evodius Mtawala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo amedai kuwa afya ya mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Aveva sio nzuri.
“Mshtakiwa wa kwanza Aveva, tangu jana amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi hali yake siyo nzuri” Wakili Mtawala.
Hata hivyo, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai ameiambia mahakama kuwa ni kweli Aveva ni mgonjwa na kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi March 22, 2018.
Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na Mashtaka matano ya uhujumu uchumi ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani (USD) 300,000.
Kamanda wa Polisi Iringa amezungumza Abdul Nondo kupatikana