Kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu‘ leo February 9, 2018 imeendelea kwa mashahidi wawili upande wa utetezi kutoa ushahidi wao ambao ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya Modestus Chambu na Mke wa Mshtakiwa wa pili Grace Malya.
Mbele ya Hakimu Mfawidhi Michael Mteite Mkuu wa Upelelezi amesema aliwaagiza ASP William Nyamakomage na Inspector Joram Magova kufuatilia mwenendo wa mkutano uliofanywa na Mbunge Joseph Mbilinyi katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge.
Jioni alipata taarifa za mkutano huo kama Afisa Upelelezi wa Mkoa kuhusu watuhumiwa kutoa lugha za fedheha dhidi ya Rais John Magufuli. Huku akiongozwa na wakili wa utetezi Peter Kibatala, Chambu amesema taratibu za uandaaji na ukamataji watuhumiwa hufanyika kisheria na kuongozwa na kanuni za Polisi yaani PGO.
Shahidi wa pili kwa upande wa utetezi Grace Malya (27) akiongozwa na Kibatala ameiambia Mahakama kuwa December 30, 2017 yeye alikuwa mgonjwa ambapo muda wa saa saba mchana alimpigia simu mumewe kuwa anaumwa ambapo mumewe alifika saa saba na dakika arobaini na tano na kumhudumia hivyo mumewe hakutoka.
Akiulizwa na Mawakili wa Serikali juu ya tatizo la kiafya Grace ameiambia Mahakama kuwa tatizo ni la muda mrefu tangu akiwa shule na kwamba anavyo vyeti. Kesi iliahirishwa kwa muda baada ya Shahidi aliyetakiwa kuwepo Mahakamani ambaye ni Mkuu wa Mkoa na Afisa Usalama kutoa udhuru. Mteite aliahirisha kesi kwa muda.
ALICHOZUNGUMZA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KESI YAKE NA HAMISA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA