Michuano ya fainali za Kombe la Dunia 2018 inaendelea nchini Urusi kwa kushirikisha mataifa 32, tayari Afrika imepoteza mataifa mawili ya Misri na Morocco kwa kutolewa kwa kukosa point hata moja lakini watacheza mchezo wa kukamilisha ratiba tu.
Hizi ndio rekodi zilizowekwa World Cup 2018
1- Luis Suarez baada ya kuifungia goli la ushindi Uruguay katika mchezo dhidi ya Saudi Arabia anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Uruguay kuwahi kufunga katika fainali tatu za World Cup tofauti 2010, 2014 na 2018 na linakuwa goli lake la 52 akiichezea Uruguay.
2- Urusi baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya 16 ya michuano ya World Cup 2018 kwa kupata ushindi katika michezo yake miwili ya mwanzo, wanaweka rekodi ya kufika hatua ya hiyo kwa mara ya kwanza katika historia toka wajigawe katika umoja wa Soviet.
3- Kwa upande wa beki wa FC Barcelona anayeichezea Hispania katika fainali za Kombe la Dunia baada ya kupata nafasi ya kucheza katika mchezo vs Iran, anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa 13 wa Hispania kuichezea taifa hilo katika michezo 100.
4- Cristiano Ronaldo baada ya kuifungia Ureno goli la ushindi dhidi ya Morocco katika ushindi wa goli 1-0, anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia kufunga magoli 85 timu ya taifa, kwa wachezaji wanaotokea bara la Ulaya baada ya Ference Puskas 84, Sandor Kocsis 75 na Miroslav Klose 71.
FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018