Shirika ya Utangazaji la Umma Afrika Kusini (SABC) imeomba msamaha kwa mwanasiasa Nkosazana Dlamini-Zuma, kwa kumzungumzia kama mke wa zamani wa Rais wanchi hiyo Jacob Zuma.
Japokuwa ni kweli mwanasiasa huyu ni mke wa zamani wa Rais Zuma amechukizwa vikali na kutambuliwa hivyo na chombo hicho cha habari badala ya kutambuliwa kama mwanasiasa jambo alilosema ni la kidhalilishaji kijinsia ambapo Mkurugenzi wa shirika hilo Nomsa Philiso ndiye iliyembidi aombe msamaha huo.
Hata hivyo baada ya kuombwa msamaha huo Nkosazana aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba “SABC inawajibu wa kutoa taarifa kwa usawa, wamesha niomba msamaha mara mbili, natumaini hakutakuwa na awamu nyingine ya wao kuniomba msamaha.”
Ulipitwa na hii? DC Gondwe katoa hekari 130 kwa Uzalendo Kwanza, zinauwezo wa kuzalisha nanasi bora zaidi ya USA