Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESBL) imeendelea na ukaguzi wa wanufaika wa mikopo katika maeneo mbalimbali ambapo leo imefanya ukaguzi katika Shule ya Sekondari Green Acres Mbezi.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukaguzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Urejeshwaji Mikopo, Fidelis Joseph, amesema wameitaka shule ya Green Acres kuhakikisha ina heshimu sheria kuhusu wanufaika wa mikopo.
Joseph amesema shule hiyo haikuonyesha nia ya kutoa makato ya waajiri wake walionufaika na mikopo tangu Bodi hiyo ilipotangaza.
Ameongeza kuwa kisheria inatakiwa mwajiri akiajiri wanufaika wa Bodi ya Mikopo, ndani ya siku 28 afikishe taarifa kuhusu waajiriwa hao katika Bodi, na kuwaambia kuwa shule hiyo walipewa taarifamiezi 5 iliyopita na hawajarejesha mikopo hiyo.
Naye Mkuu wa shule ya Green Acres, Ntipoo Resa amesema wameupokea ujumbe wa HESBL na wanaufanyia kazi na kueleza hadi kufikia kesho watahakikisha waajiriwa wapya na wa zamani ambao hawajarejesha mikopo yao wataakatwa.
BREAKING: Meya DSM ajibu kuhusu dereva wake kudaiwa kutaka kufanya fujo ofisi za CCM