Upande wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake, lipo kwa DPP ambapo wanasubiri kibali ili waiendeshe kesi hiyo.
Washitakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga ambao wakikabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.
Wakili wa Serikali, Vitalis Peter amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa, lakini jalada la kesi lipo kwa DPP wanasubiri maelekezo na kibali kutoka kwa DPP ili kuendesha kesi hiyo ambapo ameomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi October 13/2017.
Umepitwa na hii? James Rugemarila na Harbinder Sethi wamefikishwa mahakamani muda huu