Ili simu ya kiganjani iweze kufanya kazi, inahitaji iwe na laini ambayo imeunganishwa na mtandao husika. Laini hii inajulikana kama SIM card, ambacho ni kifupisho cha Subscriber Identity Module kwa lugha ya kiingereza.
Sheria inataka mtumiaji anayenunua au kupata laini ya simu kuisajili kwa majina yake halisi. Kwa
mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektoniki na Posta (EPOCA) ya 2010, adhabu ya kutokufanya hivyo ni shilingi 300,000 au kifungo miezi mitatu.
Hakikisha taarifa unazotoa wakati wa usajili ni za kweli. Ni kosa la jinai kutoa taarifa za uongo, na
inapothibitishwa mahakamani, adhabu kali hutolewa ikiwa ni pamoja na faini, kifungo au vyote viwili. Kuthibitisha usajili wako, piga *106#.
MWONGOZO KWA WATUMIAJI WA HUDUMA NA BIDHAA ZA MAWASILIANO 19
Ni muhimu kuhakikisha kwamba kitambulisho chako ndicho kinachotumika katika usajili wa laini.
Vitambulisho ambavyo vinakubalika ni:
1. Kitambulisho cha Taifa.
2. Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
3. Pasi ya Kusafiria.
4. Kitambulisho cha Mpiga Kura.
5. Leseni ya Udereva iliyotolewa Tanzania.
Ni vyema kuchagua mtoa huduma ambaye atakidhi matarajio yako na ambaye una imani kuwa atakupa huduma bora kwa gharama unayoimudu. Ujiunge na mtoa huduma ambaye atakuwa tayari kukuhakikishia haki zako, ikiwa ni pamoja na haki ya kuwasilisha malalamiko na kupata suluhisho.