Katika hali ya kushangaza Waziri Mkuu Abdoulaye Idrissa Maiga na Baraza la Mawaziri nchini Mali jana December 29, 2017 waliandika na kukabidhi barua za kujiuzulu kutoka kwenye baraza hilo.
Hata hivyo wakati serikali inatoa taarifa hii kwa vyombo vya habari hawakusema sababu ya baraza hilo la mawaziri kufikia uamuzi huo wa kujiuzulu na kwamba hivi karibuni Rais Ibrahim Boubacar Keïta wa nchi hiyo atatangaza baraza jipya la mawaziri.
Waziri huyu Mkuu aliyejiuzulu alikuwa anatarajia aidha kuwa Mkurugenzi wa Kampeni za Urais wa Keita akigombea Urais kwa awamu nyingine mwaka 2018 au yeye mwenyewe kugombea kiti hicho.
Inaelezwa kuwa Rais Keïta akichagua baraza jipya la mawaziri litakuwa ni la tano tangu alipoingia madarakani kama Rais mwaka 2013 na pia inaelezwa kuwa kipindi hiki chote serikali yake imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kiusalama zinazofanywa na Wanamgabo wa Kiislam kuvamia vikundi vya Maaskari wa Umoja wa Mataifa na raia.
Ulipitwa na hii? Agizo la Waziri Nchemba kama huna kitambulisho cha utaifa
Matukio ambayo Kamanda wa Polisi Mwanza Msangi hawezi kuyasahau kwa mwaka 2017