Wiki moja imepita tangu limetokea shambulio la risasi lililofanywa na kijana wa miaka 19, Nikolas Cruz, alilolifanya katika shule aliyokuwa akisoma kabla ya kufukuzwa iitwayo Marjory Stoneman Douglas High School iliyopo Parkland Florida, na kuuwa watu 17.
Watu mbalimbali nchini humo ikiwa ni pamoja na Wanafunzi wenyewe wamepaza sauti zao kushawishi Serikali yao kudhibiti na kuweka ukomo kwenye mashambulio ya risasi kwa kubadili sheria yake ya umiliki wa silaha.
Hatahivyo Rais Donald Trump ameeleza kuwa kuwapatia Walimu silaha kutasaidia kuzuia mashambulio ya risasi yanayofanyika mashuleni kwani wataweza kukabiliana na washambuliaji haraka kabla hayajatokea maafa makubwa.
Watu 8 wamekamatwa wakiwa Lita 4,000 za Gongo ndani ya Ziwa Victoria
Aliyekuwa Mgombea Ubunge Siha apanga kwenda Mahakamani kupinga Matokeo