Inawezekana umewahi kusikia habari za wataalamu mbalimbali wakieleza jinsi gani mvinyo yaani ‘wine’ ina manufaa kwenye mwili wa binadamu kiafya.
Wanasayansi wa nchini China miezi ya hivi karibuni wameonesha kuwa kunywa glasi moja ya mvinyo yaani ‘wine’ kila siku hupunguza hatari ya kifo cha mapema kwa mara tano.
Sasa wataalamu wengine wamekuja na hii nyingine kuhusu mvinyo kwa kueleza kuwa mvinyo mwekundu una kemikali ambazo zinakabiliana na matatizo ya kuoza kwa meno na ugonjwa ufizi.
Watafiti wameeleza kuwa mchanganyiko wa Kemikali unaotengeneza kinywaji hicho, ambao unaofahamika kama polyphenols, husaidia kumaliza kuwamaliza vimelea (bakteria) ambao wako kinywani.
Baba Mzazi wa Akwilina aomba kuonana na JPM, amesema ana siku 4 hajaoga
Aliyekuwa Mgombea Ubunge Siha apanga kwenda Mahakamani kupinga Matokeo