Wasanii wa Bongo Movie wanaounda Kundi la Uzalendo Kwanza wenye lengo la kutembea Tanzania nzima kuhamasisha watanzania kuwa wazalendo na kupenda vya kwao, walisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Tanga na kukutana na mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shegela.
Kikundi cha Uzalendo Kwanza ambacho kimekuja Tanga na kutoa msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya Tsh milioni 29, baada ya hapo wameoneshwa ukumbi mpya wa Cinema na RC Shegele uliyopo Tanga na kuambiwa huu ndio ukumbi mkubwa na kisasa wa kwanza Afrika Mashariki.
VIDEO: Mastaa BongoMovie wanaounda Uzalendo Kwanza safarini Tanga