Zikiwa zimepita siku chache tangu Afisa Tarafa wa Themi Arusha Felician Mutahengerwa kupiga marufuku zoezi la akina mama kufanya biashara wakiwa na watoto leo February 2, 2018 umefanyika msako na kukamata watoto zaidi ya 30.
Baada ya zoezi hilo Mutahengewa ameeleza kuwa lengo la tamko hilo lilikuwa ni kuhakikisha watoto wanakwenda shule badala ya kushinda Sokoni na mitaani wakifanya biashara jambo ambalo mara nyingi huwasababishia kujifunza tabia za makundi yasiyofaa.
Ameongeza kuwa yupo mama mmoja aliyejitokeza kumchukua mtoto wake baada ya kukamatwa na akaeleza kuwa mtoto huyo ni sugu na yeye mwenyewe tu hataki kwenda shule jambo lililosababisha kuandikishana makubaliano baina ya mama huyo na ofisi ya tarafa hiyo kuhakikisha mtoto huyo anakwenda shule vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
‘Afya ya Rugemarila, Seth zinatia mashaka’ Wakili