Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nsha leo January 11, 2018 akiwa katika uzinduzi wa shule ya msingi Enyorata Ereko wilayani Ngorongoro amesema serikali inatenga Tsh Bilioni 23 kila mwezi kwa ajili ya elimu bure.
Ameongeza kuwa wanafunzi katika eneo hilo wamekuwa wakitembea kilometa 28 kwenda na kurudi kutoka shule suala linalofanya mwanafunzi kutumia takribani robo tatu ya siku nzima ili kwenda na kurudi kutoka shule na kubakiwa na masaa machache ya kusoma.
“Kama hii shule isingekuwepo kuna wanafunzi ambao wasingeenda shule hata siku moja, jografia ya eneo hili ni pana sana na kuna wanafunzi ambao wasingeweza kwenda umbali mrefu.” – Ole Nasha
Wafanyabiashara wa Zanzibar wakiri kusafirisha dhahabu ya Tsh Mil 989 bila leseni
‘Lowassa amekata Kiu yake, tunamshukuru Rais JPM’ Mrisho Gambo