Leo February 14, 2018 Kutoka Afrika Kusini stori inayoendelea kushika headlines ni inayomhusu Rais wa Taifa hilo anayeandamwa na kashfa, Jacob Zuma ameibuka na kusema kuwa hajafanya lolote baya na haoni sababu ya kuondoka haraka katika nafasi yake hiyo.
Zuma amesema hayo baada ya Chama chake cha African National Congress (ANC) kutangaza kuwa itakwenda kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye, kesho Alhamisi.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75 amekuwa kwenye shinikizo kubwa la kumtaka kujiuzulu kutokana na madai mengi ya kuhusishwa na rushwa.
Akizungumza Zuma amesema: “Siyo haki na sawa kwangu katika suala hili lililoibuliwa,” alikiambia Kituo cha runinga cha SABC wakati wa mahojiano marefu ambayo hayakutangazwa. “Hawakuweza kunipatia sababu zozote.”
Kamanda Mpinga ametaja Waliokamatwa na Meno ya Tembo yenye Thamani ya Milioni 33