Ikiwa leo Club ya Yanga kupitia kwa Meneja wake wa Idara ya Habari na Mawasiliano Ally Kamwe kutangaza kuzindua documentary maalum kwa ajili ya kutunza kumbukumbu ya vizazi vijavyo.
Na katika Uzinduzi huo wa Documantary ya Mabingwa hao wa Soka leo pia wametangaza hafla hiyo itahudhuriwa na msanii wa Bongo Flevani, President wa WCB, Diamond Platnumz siku ya Jumatatu Agosti 7, 2023 katika Kumbi ya Century Cinemax iliyopo Dar Free Market jijini Dar es Salaam.
TAZAMA KIONJO CHA DOCUMENTARY YA YANGA SC, MAYELE NDANI, FEISAL ATAJWA, ‘YANGA BINGWA’