Ikiwa Club ya Young Africans wameandika rekodi nyingine ya kuchukua kombe la Shirikisho la Azam Sports katika fainali iliyochezwa leo Juni 12, 2023 Mkoani Tanga katika Dimba la Mkwakwani baada ya kuibuka kwa ushindi wa goli moja dhidi ya Azam FC.
Sasa Uongozi wa timu hiyo imetangaza rasmi kuwa June 13, 2023 kutafanyika shamra shamra za kusherehekea Ubingwa na Mafanikio ya timu yao wa msimu huu huku wakiwataka wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa timu hiyo kuungana nao katika viunga majira asubuhi saa tatu Karume- Msimbazi kisha kumalizika katika Makao Makuu ya Young Africans SC Jangwani Dar es Salaam.
Parade hiyo ya Mabingwa wa kihistoria itasindikizwa na msanii na mmiliki wa leo ya WCB, Diamond Platnumz ambae atawaimbia na kuwachezea mashabiki wa Young Africans watakaofika Jangwani Makao Makuu Dar es Salaam.