Nyota wa Bongo Flava, Diamond Platnumz ameshirikishwa katika “Mixtape” mpya ya rappa kutoka nchini Marekani, YG “Just Re’d Up 3” inayotarajiwa kutoka ijumaa ya wiki hii, Agosti 16, 2024.
Platinumz ameshirikishwa katika wimbo namba saba (07) kwenye “Mixtape” hiyo, wimbo unaitwa “Street Love” habari njema ni kuwa huenda mtayarishaji Mustard akawa miongoni mwa waliotayarisha albamu hii.
Wasanii wengine walioshirikishwa katika “Mixtape” hiyo ni Ty Dolla Sign, Saweetie, G Hebro, Mozzy, Lil Yatch na wengineo, msanii huyo alianza kuachia “Just Re’d Up” mwaka 2011 ikifuatiwa na “Just Re’d Up 2” mwaka 2013.
Platnumz na YG walionekana mwaka jana mwishoni wakirekodi video ya wimbo wao wa pamoja huko nchini Marekani, msanii huyo ameachia video tatu mpaka sasa kwenye “Mixtape” hiyo “knocka” “stupid” na “love make”.
Kushirikishwa kwa Platnumz kwenye “Mixtape” hii kunafungua milango ya muziki wa Bongo Flava kupenya kimataifa baada ya msanii huyo kuingia kwenye chati za Billboard, Afrobeats Chart, collabo na Jason Derulo na sasa kwenye kazi ya YG.