Mtandao wa CIA’S World Fact umetoa list ya nchi zenye idadi kubwa ya watu wanene duniani ambapo Amerika ya Kaskazini imeongoza kuwa na idadi kubwa ikifuatiwa na Asia ambapo Qatar na Kuwait zimeonekana kuongoza kuliko nchi nyingine huku barani Afrika kukiwa na idadi ndogo ya watu wanene ukilinganisha na maeneo mengine duniani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo zaidi ya 75% ya watu katika nchi hizi wana uzito uliopitiliza huku wanawake wakiongoza kwa unene ukilinganisha na wanaume katika nchi za kiarabu wakati Canada, Marekani na Australia wanaume wanaongoza kwa zaidi ya 25% dhidi ya wanawake.
Shirika la Afya Duniani ‘WHO’ limesema sababu za nchi hizi kuwa na idadi kubwa ya watu wanene hazihusiani na Uchumi mkubwa katika nchi hizo bali upatikanaji wa vyakula visivyokuwa na virutubisho ambavyo wanakula hasa kutoka viwandani ukilinganisha na nchi za Afrika.
VIDEO: Umepitwa na hii ya Interview ya Diamond kuhusu mzazi mwenzake Zari siku mbili kabla ya kifo chake?Bonyeza play kutazama