Katika kutatua changamoto ya Ajira Nchini Kampuni ya rangi ya Didas inalengo la kutoa Fursa kwa vijana kufanyabiashara na kuajiri kujikimu na hukosefu wa ajira.
Niwakati wa vijana kupambana na kuchangamkia fursa za ajira katika kujiajiri wenyewe na kuacha kuwa tegemezi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya rangi ya ‘DIDAS’ Daudi Wambura amesema rangi hiyo imekuja kuleta mapinduzi ni tofauti na zingine zinachubuka na zikipata maji kwenye ukuta zinapauka na kupoteza mwonekano halisi lakini yetu ni tofauti.
“Kwa kuwa rangi zetu na rangi zingine zinaendana na hali ya hewa ya nchini kwetu, rangi ya Didas ni bora inadumu kwa muda mrefu haipauki wala kufuba rangi zenye ubora zinazoendana na gharama wanazotoa kulingana na nyumba zao sio kumlaumu fundi.”
“Tutatumia fursa hii kutoa ajira kwa vijana katika kufikia malengo yetu ya tanzania ya Viwanda hivyo tunatengeneza rangi na nzuri zinazoendana na soko lilivyo nchini.” amesema Wambura