Mwanamuziki wa muziki wa hip-hop Sean “Diddy” Combs amenyimwa dhamana tena baada ya mawakili wake kubishana kwa mara ya pili kwamba anapaswa kuachiliwa kutoka kwenye hali “ya kutisha” ya jela wakati akisubiri kesi ya biashara ya ngono inayomkabili.
Jaji wa shirikisho mjini New York alimuweka rumande mwanamuziki huyo siku ya Jumanne baada ya waendesha mashtaka kudai kwamba kulikuwa na “hatari kubwa ya [mshukiwa] kutoroka”.
Bw Combs, 54, alikamatwa wiki hii, akishutumiwa kwa kuendesha biashara ya uhalifu kuanzia mwaka 2008 iliyohusisha dawa za kulevya na unyanyasaji ili kuwalazimisha wanawake “kutimiza tamaa zake za ngono”, kulingana na waendesha mashtaka.
Combs amekana mashtaka yote.
Kwa mujibu wa waendesha mashtaka wa Diddy wamesema wakati nyumba za mkali huyo zilizopo Los Angeles na Miami zilipofanyiwa upekuzi na Maafisa Usalama mwezi Machi mwaka huu, ndani kulikutwa na vitu kama vile dawa za kulevya zaidi ya chupa 1,000 za mafuta ya watoto na vilainishi.
Mbali na hayo, utakumbuka awali baada ya msako zilitolewa taarifa ya kuwa ndani kumefungwa kamera za siri.
Ikumbukwe mkali huyo alikamatwa jana Jumanne Septemba 17, 2024 na kutupwa mahabusu, kwa taarifa zilizopo sasa amenyimwa dhamana na Jaji wa Mahakama ya Shirikisho ya Lower Manhattan, hivyo amepelekwa kwenye gereza ambalo msanii mwenzie R. Kelly ndipo anatumikia kifungo chake.