Mshambulizi wa zamani wa Chelsea Diego Costa amesajiliwa na klabu ya Grêmio ya Brazil kama mchezaji huru.
Costa, 35, aliondoka Botafogo mwezi Disemba miezi minne tu baada ya kujiunga na klabu hiyo. Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uhispania, Costa mzaliwa wa Brazil amekubali kujiunga na Grêmio, klabu yake ya 12 ya kulipwa, hadi mwisho wa msimu.
“Yeye ni Mhispania, lakini ana damu ya Brazil na mataji popote alipokuwa! Diego Costa anawasili kuimarisha mashambulizi ya Grêmio,” ilisema taarifa ya klabu.
Grêmio walikuwa wanataka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji kufuatia kuondoka kwa fowadi wa Uruguay Luis Suárez, ambaye alijiunga na Inter Miami mwezi Desemba baada ya kufunga mabao 27 katika mechi 52 alizocheza nchini Brazil.