Ni zaidi ya wiki mbili zimapita tangu yaliposimamishwa matangazo kupitia mfumo wa analogy na kuanza kwa mfumo wa digital kama ambavyo tuliona TZ miaka mitatu iliyopita.
Vituo vitatu vya television vilivyozimwa wiki tatu zilizopita vitarejea hewani leo alhamisi kuanzia saa 12 na nusu jioni.
Vituo hivyo ni Citizen TV, KTN, NTV vimekuwa kwenye malumbano na Serikali kuhusu kuhamia mfumo wa digital na kufikia hatua ya kwenda Mahakamani kutafuta suluhu.
Hata hivyo mahakama iliamua kuwa vituo hivyo havikuwa na la kufanya zaidi ya kukubaliana na uamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano kuhamisha matangazo hayo kutoka mfumo analogy kwenda digital.
Vituo hivyo vya TV viliomba Serikali kuvipa muda zaidi ili waagizie ving’amuzi vyao kutokana na kampuni zilizopewa leseni kurusha matangazo ya digital kulalamikiwa kutozwa malipo ya juu.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook