Leo March 31, 2018 moya ya stori ninayokusogezea ni kutoka katika Chama cha upinzani nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo UDPS kimemtangaza Felix Tshisekedi kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu wa rais Decemba 23. 2018.
Akizungumza Kinshasa katika ofisi za chama hicho msemaji wa UDPS Peter Kazadi amesema UDPS imeamua kuweka mapambano yake vizuri kwa kumkabidhi jukumu hilo Felix Tshisekedi Tshilombo kuwania nafasi ya urais wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Mkutano mkuu wa chama hicho pia ulimpitisha Tshisekedi kuwa mwenyekiti wa chama cha UDPS kwa kura 790 kati ya 803 ambayo ni asilimia 98 ya kura zote.
Felix Tshisekedi ambaye sasa anachukua nafasi baba yake Etienne Tshisekedi , aliyefariki dunia February 2017, baada ya kutangazwa amesema hatimaye atafanikisha ndoto za waliokuwa waasisi ikiwa uchaguzi utafanyika baadae mwaka huu.
MAGAZETI LIVE: Askofu: ”2020″ chagueni Mtu sio Chama, Bombadier aliyofichua Lissu yaachiwa