Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kilimanjaro imewafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Hai, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mjini Melkizedeck Oscar Humbe aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na Valentino Molleli mtunza hazina wa Hai na kusomewa makosa manne
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Suzan Kimaro amewasomea mashtaka manne ambayo ni kutumia madaraka vibaya, wizi wakiwa watumishi wa umma, matumizi ya nyaraka za kughushi kumdanganya mwajiri pamoja na ufujaji na ubadhirifu.
Watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa ya ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milion 27.7 ambapo wanadaiwa kutenda makosa hayo mwaka 2014.
Kesi hiyo imehairishwa na watuhumiwa wapo nje kwa dhamana hadi February 15, 2018 ambapo watuhumiwa watakuja kusomewa maelezo ya awali.
Mfanyakazi wa TRA alieishi kifahari na magari 19 kafikishwa Mahakamani.