Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya taarifa ambayo ipo kwenye magazeti ya leo ni pmoja na hii kutoka gazrti la jambo leo yenye kichw cha habari, ‘Nyama choma ya baa hatari’
#JamboLEO Nyama choma ya baa yatajwa kuwa hatari kutokana na ukiukwaji wa taratibu kuanzia zinapoandaliwa hadi anapopelekewa mlaji pic.twitter.com/gUfJpshkF7
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
Gazeti la Jambo leo lmeripoti kuwa watu wanaokula nyama choma kwenye baa wako hatarini kuathirika kiafya kutokana na ukiukwaji wa utaratiu kuanzia zinapoandaliwa hadi anapopelekewa mlaji.
Jambo Leo imeeleza kuwa uchunguzi uliofanywa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania ‘TFDA’ umebaini kuwa wanokula nyama hasa baa wako haratarini kuathirika kiafya kwa namna mbalimbali kwa sababu hiyo TFDA imependekeza kuwa wanaoandaa nyama hiyo wanapaswa kuabadili tabia kwa kuhakikisha imekaguliwa na mabwana afya, inachomwa kwa uangalifu na anapelekewa mteja ikiwa bao ya moto.
Gazeti hilo limeeleza kuwa kwa kuwa nyama ni sehemu ya vyakula ambayo inaonekana kuvuta hamu ya kula kwa watu wengi, wanywaji baa hupendelea kunywa nyama zaidi kama moja ya kiamasidhio cha starehe ya kupata kilevi, nyama inayotumiwa zaidi ni ile inayotokana na ng’ombe, nguruwe, mbuzi, kuku na kondoo hata hivyo inaweza kuchafuliwa na vimelea mbalimbali vya maradhi endapo kanuni bora za usafi hazitazingatiwa wakati wa uaandaji na utunzaji wa nyama hiyo.
TFDA inaeleza kabla ya kuliwa nyama huweza kuandaliwa kwa njia ya kuchomwa kwenye jiko la mkaa kuni, jiko la umeme au gesi hadi hapo itakapobadiliaka rangi kuashiria kuwa imeiva.Utarishaji wa aina hii hupendwa na walaji wengi kwa kuwa unaaminika, hii ni baada ya kupika kwa kutumia maji au mafuta yake hivyo kuwa na radha nzuri.
Utayarishaji wa nyama kwa njia ya kuchoma hufanyika kwa wingi kwenye maeneo ya baa, hotel, migahawa na hata majumbani, hata hivyo baadhi ya tafiti zinaonyesha mara nyingi nyama inayochomwa haivi vizuri na hivyo kubaki na vimelea vya maradhi ambavyo ni hatari kwa afya ya mlaji, hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi hasa nyama inayochomwa inapokuwa haikukaguliwa na kupitishwaa na mamlaka husika kuwa inafaa kwa matumizi ya binadamu.
Source: Jambo Leo
Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa kutoka magazeti ya Tanzania leo September 23 2016
#MWANANCHI Polisi yalegeza masharti ya kudhibiti shughuli za kisiasa, yaruhusu mikutano ya ndani ya vyama na ya wabunge kwenye majimbo yao pic.twitter.com/W0rJfjfnPj
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#MWANANCHI Ujenzi wa daraja refu kuliko yote nchini la Salender kuanza June mwakani ukilenga kupunguza msongamano wa magari DSM pic.twitter.com/NsaMNRLRSp
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#MWANANCHI Imeelezwa kuwa kisukari, shinikizo la damu na uzito mkubwa ni miongoni mwa maradhi yanayozalisha matatizo ya figo pic.twitter.com/enxbm5rZ1z
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#MWANANCHI Idadi ya wanaokamatwa kwa kumkashifu Rais Magufuli imeongezeka baada ya mhadhiri wa chuo kikuu MUCE, Dk. Oscar Magava kukamatwa pic.twitter.com/MaAwQSui6e
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#MWANANCHI Hospitali ya Mloganzila inatarajiwa kutoa huduma za afya kwa mfumo wa digitali kuanzia January 2017 itakapozinduliwa rasmi pic.twitter.com/aZF9G0tMZ1
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#NIPASHE Licha ya kuamriwa kuilipa Standard chartered bil 320, wanasheria TANESCO wanaona shirika limeokoa zaidi ya bil 540 ktk hukumu hiyo pic.twitter.com/ZOcyeVSmAA
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#NIPASHE Magonjwa ya saratani ya shingo ya kizazi, tezi dume, matende, moyo, figo na shinikizo la damu yatajwa kuwasumbuwa watanzania wengi pic.twitter.com/hrA4OnwB7N
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#JamboLEO Coast Textiles yawasilisha pingamizi la awali mahakama kuu dhidi ya ombi la BoT kutaka amri ya kuilipa kampuni hiyo bil 92 ifutwe pic.twitter.com/7TAsSzYetP
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#JamboLEO Idadi ya watalii waliotembelea hifadhi za taifa kuanzia 2007 hadi 2016 imeongezeka kutoka 445,567 hadi 547,154 pic.twitter.com/lKV5ej8JeO
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#JamboLEO Waziri Lukuvi kuweka wazi chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji iliyodumu kwa miaka 27 baada ya kusoma taarifa ya uchunguzi pic.twitter.com/UL2NyqqrKO
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#JamboLEO Mchungaji raia wa Zambia, Judith Namwinga amesema Rais Magufuli ni kiongozi hodari kuliko wengine Afrika pic.twitter.com/24Zl3BUqRU
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#MTANZANIA Bodi ya mikopo elimu ya juu imesema haiwezi kutoa mikopo kwa waombaji wapya walioomba baada ya TCU kushusha viwango vya udahili pic.twitter.com/c5RKoUQPvE
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#MTANZANIA Serikali kufunga mfumo wa vidhibiti mwendo kwenye mabasi yote yanayokwenda mikoani kupunguza ajali za mara kwa mara pic.twitter.com/MwxgI5Aqlo
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#MTANZANIA Imeelezwa shule 353 za msingi na sekondari ziliathiriwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera lililotokea September 10 mwaka huu pic.twitter.com/I0l9Dube8b
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#HabariLEO TANESCO kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kulitaka shirika hilo kuilipa bil 311 Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong pic.twitter.com/QP1SoERLz2
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#HabariLEO TZ yatajwa mfano kwa ukusanyaji mapato, imeelezwa mfumo wa kidijitali unaweza kuiongeza mapato ya kodi hadi trilioni 1 kwa mwaka pic.twitter.com/WnlsX7paaW
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#HabariLEO Serikali yaokoa trilioni 16 kuanzia July 2014 hadi June 2015, fedha ambazo ingezilipa kama ingenunua gesi hiyo nje ya nchi pic.twitter.com/lmpJwlhc0C
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#MWANASPOTI Mwafrika tajiri zaidi, Aliko Dangote amepanga kuinunua klabu ya Arsenal ndani ya miaka minne ijayo pic.twitter.com/ybMoI9s7By
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
#JamboLEO Nyama choma ya baa yatajwa kuwa hatari kutokana na ukiukwaji wa taratibu kuanzia zinapoandaliwa hadi anapopelekewa mlaji pic.twitter.com/gUfJpshkF7
— millardayo (@millardayo) September 23, 2016
ULIKOSA HUU UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA TANZANIA KUTOKA AYO TV SEPTEMBER 23 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI