Leo December 22, 2017 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka ametangaza kamati ambayo ina jumla ya wajumbe nane, ikiongozwa na Mwenyekiti Maryam Chaulembo ambayo itafuatilia vitega uchumi na rasilimali za umoja huo.
“Kamati hii baada ya kutangazwa leo, itaanza kazi mara moja na watapewa mwongozo ndani ya kipindi kifupi sana wawe wamekwisha kamilisha kazi yao, na pindi watakapomaliza kazi hii Watanzania watapata taarifa ya kilichobainika.” – Shaka Hamdu Shaka
“Nimepigwa vita sana, siogopi ” – Katibu Mkuu UVCCM