Aliyekua Mwenyekiti wa tume ya taifa ya kukusanya maoni ya katiba Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba leo kupitia kipindi cha dakika 45 cha ITV amezungumza mambo mengi sana ya msingi kuhusu muungano yakiwemo yale yanayoihusu Tanzania bara na Tanzania visiwani,haya ni miongoni mwa mambo hayo.
1.Mchakato umeanza nadhani kwa kusuasua bunge limechukua muda mrefu kutengeneza kanuni na wameanza haikua mwanzo mzuri mpaka imefika mahali wamefarakana lakini tunaendelea na mchakato bado matumaini yapo.
2.Sisi tulipoenda kufanya kazi tulienda kukusanya maoni ya Wananchi tulichukua maoni ya Wananchi kwa ujumla tukapeleka mapendekezo ambayo tuliamini ni ya kuwaunganisha Wananchi tulichotegemea ni kwamba Bunge nalo lingekwenda na muelekeo huo lakini toka mwanzo likaonekana bunge limejiunda katika makundi badala ya kuanagalia suala lenyewe la maoni ya Wananchi likaanza kuonekana mgawanyiko toka mwanzo wanatengeneza kanuni.
3.Wakati tunakabidhi rasimu ya kwanza nilisema ili tuendelee na muungano inahitaji ukarabati mkubwa na tukasema kwa tathmini ya tume itakua ni vigumu sana kufanya ukarabati huo ndiyo maana tumependekeza serikali tatu.
4.Tulipopita kwa wananchi walikua wanauzungumzia muungano walisema tuuboreshe muungano lakini wakati wote wakasema tatizo letu ni muundo wengi walizungumzia muundo tulionao,tulianza kuorodhesha mambo yote yaliyosemwa na bara na visiwani.
5.Zanzibar wamekwenda wamepitisha sheria wanasema sheria zozote zitakazotungwa na Bunge la Muungano haziwezi kutumika Zanzibar mpaka zipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi maana yake Baraza la wawakilishi limekua kubwa kuliko Bunge la Muungano.
6.Tuna mahakama ya rufaa ina madaraka nchi nzima wameenda wametunga wamebadili katiba yao wamesema kuna mambo fulani fulani haki za binadamu,mashauriano yanayotoka kwenye mahakama za kazi na kutafsiri katiba ya Zanziba hayo hayatakuwa kwenye madaraka ya muungano lakini kwenye katiba ya muungano imesema katiba hii ina mamlaka yote.
7.Tusiingize jeshi kwenye mambo ya siasa za makundi Jeshi ni la nchi,mimi nimetumikia nchi hii nimekua kwenye utumishi wa umma kwa muda mrefu mpaka nikawa Waziri Mkuu na nilipokuwa Waziri Mkuu nilikua nazunguka nchini kuangalia shughuli za kimaendeleo na kila nilipoenda kama kuna kambi ya jeshi karibu nilikua naenda kukaa nao.