Karani wa Sensa Kata ya Majimoto Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi Kenan Kasekwa amevamiwa na kuporwa kishikwambi cha kutunzia kumbukumbu za Sensa.
Akithibitisha tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Catherine Mashala amesema Karani huyo ambaye ni Mwalimu alivamiwa na Mtu ambaye alivunja kitasa na kuingia chumbani kisha kubeba kifaa hicho, fedha kiasi cha Tsh. 760,000, radio na vitu vingine.
“Inavyoonekana alipuuliza dawa ya kuwalaza usingizi yeye na Familia yake, yule Mwizi alingia chumbani akabeba ka lasketi, kishikwambi, fedha alizozikuta, simu na radio aina ya sabufa”
Mashala amesema baada ya tukio hilo alitoa taarifa kituo cha Polisi ndipo Polisi walipofuatilia na kufanya msako na kumkamata Mtuhumiwa.
Kwa stori kamili unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.