Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amewapa somo Wasimamizi wa Miradi Wizara ya Afya juu ya umuhimu wa kuhakikisha Miradi ya Maendeleo inaimarisha Maisha na uasalama wa Wananchi kwa kukidhi mahitaji kijamii, na kuleta matokeo chanya yenye manufaa na tija kwa jamii na sio kuiangamiza.
Dkt. John Jingu, amesema hayo Mei 23, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akifunga kikao kazi cha Kuboresha utendaji kazi kilichokutanisha Wakurugenzi, Wakurugenzi wasaidizi, Mameneja, Wakuu wa progarmu, waratibu wa Miradi na baadhi ya Maafisa wanaosimamia utelezeji wa Miradi hiyo kutoka Wizara ya Afya.
“Kwenye utekelezaji wa miradi hasa kwenye sekta hii ya Afya ambayo inamgusa mwananchi moja kwa moja ukifanya makosa tu au ukifanya ka uzembe inawezekana watu wakapaoteza maisha ama wakapata ulemavu wa maisha hivyo Makosa kwetu hayakubaliki sababu Madhara ya Makosa kwenye sekta yetu ni hatari kwa jamii” amesema Dkt. Jingu.
Amesema kwa kuliona hilo Wizara ya Afya imeamua kufanya Kikao kazi hiki ili kuboresha utendaji kazi kwa kuwafundisha namna bora ya utekelezaji wa Miradi na kuipusha jamii na Makosa yanayo zuilika.
“Kama watumishi wa umma ni Muhimu kukumbushana, kufundishana na kuelekeza umuhimu na wajibu wetu ni upi, Nini kinatarajiwa kutoka kwetu baada ya hapo ukikosea kwa makosa ambayo yanazuilika hapo unatakuwa umefanya kusudi nasi hatutalifumbia macho hilo” aliongeza Dkt. Jingu
Dkt. Jingu pia amatumia fursa hiyo kuwasihi watumishi wa umma na wale wasio wa umma kuhusu suala la Maadili.
“Tuzingatie Maadili ya kazi zetu, Maadili ya kazi zetu kila mtu kwa eneo lake na maadili ya Utumishi wa Umma Kwa ujumla wake, hata ukiwa Mtumishi wa ajira za mkataba wa siku moja ni lazima ufuate Maadili ya Utumishi wa Umma kwani Maadili haya yanatuhusu wote”
Nae Afisa wa Serikali Haika Msuya aliyetoa mada katika kikao hicho, amewasihi washiriki hao wa kikao kazi hicho kuendelea kufanya kazi kwa Bidii ili kukidhi mahitaji ya wanachi walio wengi kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala Wizara ya Afya Issa Ng’ambi licha ya Kumshukuru Katibu Mkuu kwa kwa kikao kazi hicho amemuomba kuwepo kwa vikao hivyo mara kwa mara na kuwafikia watumishi wengi zaidi ili kujengana
Kikao hicho ambacho kimeanza Mei 22, 2023 kimefanyika Bunju Jijini Dar es Salaam ambapo awali kilifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe ambapo kwa jana na leo Mada mbalimbali zimewasilishwa kutoka ofisi Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma na Mamlaka zingine za Serikali.