Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema Dkt. John Samwel Malecela ni kiongozi wa kuigwa Afrika kutokana na kuwa miongoni mwa viongozi saba wenye busara kutoka nchi za jumuiya ya madora waliosaidia kuleta uhuru Afrika ya Kusini.
Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati akitoa pongezi kwa Waziri mkuu mstaafu na makamu wa kwanza wa Rais Dkt. John Samwel Malecela kwa kutimiza miaka 90 sherehe iliyofanyika nyumbani kwake Kilimani jijini Dodoma
“mzee Malecela ametoa mchango mkubwa katika ukombozi wa kusini mwa Afrika alipokuwa Waziri wa mambo ya nje na pia alipokuwa kwenye kamati ya kuondoa ukoloni ya umoja wa mataifa lakini kubwa la kujivunia alikuwa miongoni mwa watu saba wenye busara kutoka nchi za jumuiya ya madola walioteuliwa na jumuiya hiyo kujadiliana na serikali ya makabulu ya Afruka ya Kusini juhudi hizo zilisaidia kuachiwa huru kwa Nelson Mandela mwaka 90 na baadae nchi hiyo ikapata Uhuru