Waziri wa viwanda na biashara Dr Ashatu Kijaja ameuagiza uongozi wa tume ya ushindani FCC kusimamia uadilifu na usimamizi wa sheria ya ushidani na kanuni zake ili isitumike kuumiza walaji na wazalishaji wadogo kwa kuwaachia wakubwa kujipangia uendeshaji wa soko na kufifisha biashara za watu wengine huku akiwataka pia wenye viwanda na wafanya biashara kujiandaa kushindana kwenye masoko ya nje ya tanzania.
Dr Kijaji ameeleza hayo kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya ushindani ambayo hufanyika kila mwaka dec 5 na kauli mbiu ya mwaka huu ikijikita zaidi katika kuzungumzia “madhara ya njama baina ya washindani kwa walaji na watumiaji”ambapo FCC imetoa mafunzo kwa wajasiriamali sehemu mbalimbali nchini kwenye kilele cha maadhimisho haya.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Fcc William Erio, amesema namna ambavyo njama baina ya washindani zinaathiri maslai na ustawi wa jamii na kuelezea maswala mahusis kuhusiana na kipengele cha local content policy aspect katika gesi na mineral subsectors na namna inavyoweza kuinua hali za wachimbaji wa madini na wafanyabiashara kwa ujumla.
Nae Mkurugenzi wa CTI ,Leodgar Tenga amesema kuwa ushirikiano wa kufanya kazi umekuwa wa tija kwani unahitaji kuwa mshindani ndio ufanye vizuri,kwahiyo Cti wamefanya kazi kubwa kusaidiwa na Fcc kuzungumza na wanachama wao.