Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia amekutana na ujumbe wa CRDB Bank ulioongozwa na Dominick Timothy, Meneja Mwandamizi (Taasisi za Serikali) ambao ulifika katika ofisi za HESLB zilizopo TAZARA jijini Dar es salaam.
Lengo la ziara hiyo lilikua ni kujitambulisha kwa Dkt. Kiwia ambaye aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB tarehe 6 Februari mwaka huu.
Katika kikao hicho, HESLB na Benki ya CRDB walikubaliana kuendeleza ushirikiano uliopo katika kutoa huduma kwa wanafunzi na wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu wanaorejesha.