Ni Februry 28, 2024 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia amekutana na ujumbe wa NBC ulioongozwa na Linley Kapya, Mkuu wa Huduma za Kibenki (Sekta ya Umma na Taasisi) ambao ulifika katika ofisi za HESLB zilizopo TAZARA jijini Dar es salaam.
Lengo la ziara hiyo lilikua ni kujitambulisha kwa Dkt. Kiwia ambaye aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB tarehe 6 Februari mwaka huu.
Katika kikao hicho, HESLB na Benki ya NBC walikubaliana kuendeleza ushirikiano uliopo katika kutoa huduma kwa wanafunzi na wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu wanaorejesha.