Msemaji wa familia ya Dkt.Pius Ng’wandu na mbunge wa jimbo la Maswa mashariki Stanslaus Nyongo ametaja sababu za mwili wa marehemu kusafirishwa kwenda DSM kwa maziko kuwa ni maelekezo aliyoacha.
Nyongo amesema marehemu Dkt. Ng’wandu tayari alikwisha chimba kaburi kwaajili ya maandalizi ya sehemu atakapohifadhiwa na kwamba wananchi wa Maswa na watanzania waelewe maamuzi hayo.