Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepiga simu kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda na kutoa salamu za shukrani na upendo kwa Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi na kuunga mkono juhudi za utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya Sita inayotokana na CCM.
Aidha, Dkt. Samia amenpongeza Mwenezi Makonda na kumtakia majukumu mema ya kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwenye ziara yake ya Mikoa 20 Back To Back.