Kivuko cha MV Magogoni kinachotoa huduma kati ya Kigamboni na Magogoni leo asubuhi kimeshindwa kutoa huduma kutokana na kamba na nanga za boti za wavuvi wanaofanya shughuli zao Kigamboni kunasa kwenye mitambo ya kuendeshea kivuko hicho.
Hata hivyo zoezi la kuondoa nanga na kamba zilizonasa kwenye mitambo hiyo ya kuendeshea kivuko hicho inaendelea kufanywa na wazamiaji na pindi tu watakapomaliza, shughuli za usafirishaji za kivuko hicho zitaendelea kama kawaida.
Kwa mujibu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ambao ndio wametoa taarifa hii rasmi wameeleza kuwa taarifa za usafirishaji zinaendelea kwa MV Kazi na MV Kigamboni na hivyo kutoa wito kwa wanaofanya shughuli za kibinadamu katika eneo hilo kuacha kwani zinaathiri sana uendeshaji wa vivuko.
Ilivyoendelea kesi ya Mhasibu wa TAKUKURU anayedaiwa kumiliki mali za Bilioni 3
MWANZO MWISHO: Kingunge asimulia alivyong’atwa na mbwa wake