Leo February 19, 2018 nakusogezea stori kuhusu Watu wawili kukamatwa na wengine wawili kufanikiwa kutoroka baada ya Jeshi la Polisi wilaya Ruangwa katika mkoa wa Lindi kufanikiwa kuwakamata kwa madai ya kutaka kuvamia kituo cha Polisi wilayani humo huku wakiwa na silaha za kivita.
Kamanda wa Polisi mkoa Lindi, Renatha Mzinga amesema kwa sasa watu hao wako chini ya ulinzi na wanaendelea kuhojiwa.
Kamanda Mzinga amesema katika msako ulioendeshwa katika wilaya ya Liwale, Polisi wamekamata silaha ikiwemo bunduki moja aina ya SMG na mapanga matatu pamoja na vifaa mbalimbali vya kuvunjia.
“Watuhumiwa hao walikuwa wakizunguka kituo cha polisi kabla ya kudhibitiwa na baadaye kufuatiliwa na kukutwa na zana hizo mbalimbali za uhalifu.” Kamanda Mzinga.
Via Azam
UTEUZI ULIOFANYWA NA RAIS MAGUFULI LEO FEBRUARY 19, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA