Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoani Arusha imemfutia mashtaka matatu Mzee Karankiyo Nassari aliyokuwa akituhumiwa nayo ya kumbaka na kumpa ujauzito Mtoto wa kaka yake aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la saba.
Akitoa uamuzi huo leo Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru Pamela Meena ameeleza kwamba upande wa mashtaka umeshindwa kithibitisha kwamba Nassari alimpa ujauzito mwanafunzi huyo.
Hakimu Meena amesema kwamba kwa mujibu wa vipimo vya DNA ambapo kati ya sampuli 15 kutoka kwa mama na 15 zilizochukuliwa kutoka kwa mtoto zilifanana lakini sampuli 15 kutoka kwa Karankiyo Nassari na 15 kutoka kwa mtoto zilifanana saba pekee hivyo kupelekea Karankiyo kutokuwa baba mzazi wa mtoto huyo.